Many People join Binance because Binance is a trusted crypto Exchange around the world. So it is time for you to start the crypto journey with Binance and earn a welcome bonus of $100 in rewards

Kumekuwepo na mitazamo hasi ambayo inatokana na wale watu ambao huwa hawataki kuumiza vichwa kujua uhalisia wa Cryptocurrency na Blockchain technology bali wako tayari kuona mafanikio ya haraka bila kujua hasara zinazokuwa zinapatikana hasa mtu anapoingia kwa pupa kwenye teknolojia mpya hasa masuala ya kifedha.

Watu wengi wapo kupotoshwa juu ya ujio huu wa Cryptocurrency wakidhani ni utapeli, mtu akisikia neno Bitcoin basi akili yake huwa inamtuma moja kwa moja kuwa ni utapeli. Kwanini hufikiria kuwa ni utapeli? Huwa wanafikiria ni utapeli kwa sababu watu wengi wamefahamu Bitcoin kupitia platforms za kitapeli zinazojulikana ponzi Schemes au Pyramid Schemes.

Platforms hizi zimeharibu watu wengi wasiwe na mitazamo chanya juu ya Bitcoin au Cryptos wakidhani vyote hivi ni utapeli, ndiyo maana sasa mtu akisikia Bitcoin au Cryptos basi moja kwa moja hufikiria kuwa ni mambo ya utapeli mpaka kufikia wakati hata muamko wa watu wengi kuanza kuifuatilia Cryptocurrency inakuwa ngumu. Mfano mzuri sasa hivi tunaojihusisha na cryptocurrency tuko zaidi ya 580 Milioni ambayo ni sawa na 5% ya watu 8 Billion kote duniani.

Mtazamo kama huu hata mimi nilikuwa nao mwaka 2018 ambao ulikuwa ni mwaka wa kuanza Sarafi yangu ya Cryptocurrencies, japo kwa bahati mbaya sana niliingia kupitia ponzi Schemes ijulikanayo BTCRACE nilikoweza kutapeliwa pesa yangu kiasi cha $1200, iliniuma sana na nilijisikia vibaya maana ilikuwa pesa yangu pekee nilivyotarajia kupata faida kwa lengo la kujua jinsi ya kuwekeza online lakini bahati mbaya sana pesa yangu yote ilitapeliwa kupitia hii ponzi Scheme ya BTCRACE.

Baada ya kutapeliwa nilikaa chini nikatafakari nikaanza kujiuliza maswali mazingira nilivyoweka pesa yangu kutoka mfumo wa Fiat Money mpaka kupitia Bitcoin. Nikawa najiuliza hii Bitcoin ni nini kwanini pesa zangu nimezibadili kutoka local currency kwenda Bitcoin. Na kipindi najiunga na hii BTCRACE pia niliweza kusajili akaunti yangu ya localbitcoins ambako ndiko nilinunua Bitcoin zangu huko na kuzipeleka kwenye platform ya BTCRACE ambayo ilituahidi kulipwa 2% kila siku ya mtaji yetu tuliowekeza(zingatia vizuri hapa nikanunua Bitcoin kutoka localbitcoins kwa mfumo wa local currency hivyo maana yake hapa pesa halali ni Bitcoin ila platform ya BTCRACE Ndiyo ilitumika kuniibia pesa zangu kwa mfumo wa Bitcoin) Hivyo basi kumbe kitu halali ni Bitcoin ili kuepusha ile dhana ya watu wengi kusema Bitcoin ni utapeli.

Hivyo basi baada ya kukaa kwa miezi kadhaa hivi kutoka ule mwaka wa 2018 mpaka kufika mwaka wa 2019 nikaanza kuwa agent wa localbitcoins sehemu ambayo ikanipa muda wa kuanza kusoma kwa kina kujua uhalisia wa Cryptocurrency huku nikisoma kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, ndipo nikabahatika kusoma whitepaper iliyonipa muongozo sahihi wa jinsi ya kujua mfumo mzima wa Cryptocurrency na siri zake zote na kujua kusudi lake la mfumo huu kuvumbuliwa. Hapo sasa nikaanza kujiona mtu mwenye furaha maumivu ya kutapeliwa $1200 yakaanza kuyeyuka taratibu, maana ilifika hutua kuanza kujua mambo mazito hasa ya Bitcoin halving kazi yake ni nini, nini umhimu wake hasa kwa wale wanaoweza kuweza Cryptocurrencies zao kwa muda mrefu. Je ni nini matunda yake yanakuwa kwa mtu mwenye subra ya muda mrefu? Nikawa nazidi kufurahi pale naanza kufuatilia vitu vingi vya uhakika kama vile Binance.

Nikafuatilia Binance ni nini? Na je inajihusisha na nini? Basi nikawa nazidi kufurahia akili ya kutaka kujua vitu vingi vya uhakika hasa vitu ambavyo ni matunda mazuri ya mimi kupenda kujisomea. Baada kufanya utafiti wangu wa kujiridhisha basi ilikuwa mwaka wa 2020 ndipo nikasaji akaunti ya Binance ili nianze kujifunza jinsi ya ku trade cryptocurrency pale Binance spot trading. Kwa maana hiyo nikawa nafanya vitu viwili vya kuwa agent wa localbitcoins halafu ni trader wa Binance spot.

Siku zikawa zinaenda kufika mwaka 2021 huku nikiwa naendelea kuitumia Binance crypto Exchange nikawa nazidi kuiamini zaidi jinsi ilivyo na mfumo mzuri wa management hasa pale nilipokuja kumuona CEO wa Binance kwa wakati ule CZ nikawa nafuatilia posts zake kule Twitter. Hicho kikawa kigezo cha mimi kuanza hata kuwajulisha rafiki zangu wa karibu kuwataarifu wakitaka kuanza Safari zao za Cryptocurrency basi ni vema waanzie Binance sehemu ambayo ni salama kwa uwekezaji wa Cryptocurrency. Mwaka huohuo wa 2021 nikaanza kutamani kuwa merchant wa Binance P2P Nikafanya application nikakubaliwa hivyo kuwa verified merchant wa kwanza na wa pekee nchini Tanzania.

Baada kuwa verified merchant Binance P2P niliona nisiwe pekee yangu nikaanza kuhamasisha wengine waweze kuwa merchant wa Binance P2P. Mpaka sasa hivi kuna merchant wengi mno nchini Tanzania hivyo nikazidi kujiona mtu mwenye furaha ambaye naonekana mtu wa pekee kuamsha watu wengine kutumia Binance P2P.

Kwa sababu ya kupenda kufuatilia mambo kwa kujisomea, niliweza kushiriki ku organize first offline event ya Binance nchini Tanzania mwaka 2022, kwangu niliona ni historia yenye heshima kubwa kuwa miongoni mwao watu wa kwanza kabisa ku organize first offline event nchini Tanzania. Yote haya yalitokea kwa sababu kuu ya mimi kuwa na imani na Cryptocurrency na kufanya utafiti ni wapi ni mahali salama pa uwekezaji wa Cryptocurrency hivyo nikawa najiamini kabisa kuwa Binance ni sehemu salama pa mtu yeyote kuanza Safari yake ya Cryptocurrencies.

Swali la kujiuliza wewe ambaye ni mgeni na Binance:

Je kwenye Crypto Exchange ya Binance utafaidika na nini endapo umesajili akaunti yako?

Zifuatazo ni faida kubwa za huduma za wewe endapo utakuwa na akaunti ya Binance. Naziorodhesha hapa chini ili ukipata muda jaribu ujisomee ujue jinsi zinavyofanya kazi na faida zake endapo utaweza kuzitumia na ikawa ndiyo mwanzo mzuri wa wewe kujua uhalisia wa Cryptocurrency pindi ukiwa na akaunti ya Binance.

1. Binance Academy ni sehemu ya kujifunza mambo ya Fourth Industrial revolution kama vile Blockchain technology, Cryptocurrency, Metaverse, IoT, Web 3, AI and other things.

2. Binance P2P ni gateway ya kubadili Fiat Money to Crypto or Crypto to Fiat Money.

2. Spot trading sehemu ya wewe kununua crypto kwa bei ya chini and then subiri bei ikiwa appreciated upate faida.

3. Binance Earn sehemu ya ku earn passive income.

4. BinanceNFT kwa ajili ya ku showcase kazi zetu za sanaa kuziuza na kununua kwa mfumo wa kidigitali zaidi.

5. Binance Pay sehemu ya kulipia Bidhaa mbalimbali kama vile flight ticket etc.

6. Binance Launchpad sehemu ya kujipatia airdrop za bure ambayo ni kama faida ya watu kujihusisha ku stake BNB.

7. Binance Square sehemu ya kuonesha ujuzi wako juu ya Cryptocurrencies pale unapoandika content au sehemu ya kujifunza fikra za wengine kupitia makala zao ambazo wanazi post Binance Square hivyo ni sehemu sahihi ya kubadilisha mawazo kutoka kwa Creators mbalimbali kote duniani.

Nina mengi ya kuandika lakini ni vema nikakutaarifu kuwa, Sehemu sahihi ya wewe ujifunze uhalisia wa Cryptocurrency ni Binance tu. Hii itakusaidia pakubwa kujua siri zilizo kwenye mfumo wa Cryptocurrency ili uondokane na dhana ya kudhani cryptocurrency ni utapeli kumbe siyo bali imeenezwa kuwa ni utapeli kutoka kwa wale ambao ni wavivu wa kujisomea kutafuta ukweli. Mimi mwenyewe nimewahi kutapeliwa kwa mara ya kwanza kwa sababu sikujua uhalisia wake. Pamoja na hayo sikuweza kueneza mtazamo hasi kuwa Bitcoin ni utapeli badala yake nikajitafakri kuwa kumbe nilitapeliwa kwa sababu ya kutojua, lakini sasa hivi najua kabisa uhalisia wake na tayari naendesha maisha yangu ya kila siku kwa cryptocurrency na hii ndiyo siri yangu kubwa kufaidika na matunda ya kupenda kujisomea.

Hivyo nakusihi sana na wewe uwe na akaunti ya Binance ndipo pana kila kitu chenye faida cha wewe usirudie tena kutapeliwa kwenye Ponzi Schemes ambazo zinaharibu pakubwa kwa kuharibu mentality ya watu wasijue uhalisia wa Cryptocurrency.

Mwisho; pia tutambue kuwa pamoja na faida zitokanazo na uwekezaji wa Cryptocurrency lakini pia kuna faida ya mtu mwenye skills za Cryptocurrency anaweza kupata ajira ya mtu kulipwa mshahara kila mwezi kupitia Crypto Exchanges mbalimbali. Mfano Binance na wao wana kitengo cha kuajiri watu wanaopenda kufanya kazi na Binance. Hizi ni miongoni mwa ajira ambazo Binance huwa wanazitoa kwa ngazi kila aina watu kupitia elimu zao kama vile ajira za watu wa sheria, Engineering, Marketing, hasa ni ajira ambazo zinaendana na elimu ya Teknolojia mpya kwenye nyakati za Fourth Industrial Revolution.

Baadhi ya ajira hizi ni Community Manager, Customer support, Content Manager, Affiliate Manager, Marketing manager

People & Culture Lead. ...

HR Specialist. ...

Project Manager. ...

Personal Assistant. ...

Marketing Specialist, APAC.

Hizi ni baadhi ya jobs ambazo Binance Huwa wanaajiri.

So kama unataka siku moja uje kuajiriwa na Binance ili uwe unalipwa mshahara kila mwezi basi ni vizuri uwe na akaunti ya Binance maana ni kipindi kigumu mno kwenye la ajira kote duniani, hivyo unapokuwa na akaunti ya Binance basi inakuwa ni mwanzo mzuri wa wewe kupata ajira kwenye Exchange ya Binance.

Mimi mwenyewe nimejikita zaidi kuwekeza kwenye Cryptocurrency na ku trade lakn kulingana na ubora wa Binance Exchange hivyo na mimi natamani sana niwe muajiriwa wa Binance kuwakilisha region yangu ninayoishi hasa ninapoona Ni Crypto Exchange ya pekee kote duniani kuwa na mfumo mzuri wa kuhakikisha usalama wa pesa za watu wengi zinabaki salama bila aina yoyote ile ya upotevu. Hivyo basi kwa ubora huu lazima mtu uwe uchu wa kuajiriwa na Binance.

Mimi niko tayari kuajiriwa na Binance je na wewe uko tayari kuajiriwa na Binance na hauna akaunti ya Binance? Basi nakusihi sajili akaunti yako ya Binance jaribu ujifunze jinsi ya ku deposit pesa zako, jinsi ya ku trade jifunze kutumia Binance Academy ili uwe na uwanja mpana wa kuajiriwa hapo baadaye na Binance.

Kumbuka makala hii ni mtazamo wangu binafsi kwa lengo la kuelimishana tu wala haihusiani na Binance hivyo ni vema ukafanya utafiti wako Binafsi kabla ya kuanza kuwekeza kwenye Cryptocurrency maana kuna hasara kubwa endapo mtu utaingia kwa pupa bila kujielimisha. Lakini kuna faida kubwa kwa wale wanaopenda kujielimisha hivyo tuache dhana ya kueneza taarifa hasi juu ya Cryptocurrencies.

Ahsante nakutakia siku njema na ya furaha kuanza Safari yako ya Cryptocurrencies na Binance. Sajili akaunti yako ya Binance leo hivi hii

#TradeNTell #Write2Earn