Haya ni maandishi ya Kiswahili yaliyopita tulishuhudia tukio kubwa na la kihistoria hapa Tanzania, Dar es Salaam—Lightning Developer Bootcamp iliyodumu kwa siku 5.
Bootcamp hii iliongozwa na viongozi mahiri kutoka Africa Free Routing, ndugu Megasley & Yasir, na ilidhaminiwa na mashirika makubwa ya kimataifa kama Human Rights Foundation (HRF), Btrust, PlanB.network, na Tether, kwa kushirikiana na familia yetu ya Bitcoin hapa Tanzania, BitcoinSafariTz.
Kwa siku 5, ma-developers walijifunza kwa kina teknolojia ya Bitcoin na Lightning Network kuanzia misingi ya protocol, jinsi ya kutengeneza wallets, hadi jinsi ya kujenga application zinazofanya kazi kwa haraka na kwa gharama nafuu.
Mwishoni mwa bootcamp, washiriki walishiriki kwenye hackathon na kutengeneza products mbalimbali ambazo zinalenga kutatua changamoto halisi za kijamii hapa Tanzania kwa kutumia Lightning Network. Hii ni hatua kubwa kuelekea kujenga suluhisho za kiafrika kwa kutumia teknolojia ya Bitcoin.
Lakini kuna jambo muhimu la kuzingatia. Asilimia kubwa ya walioshiriki walikuwa wanaume, na idadi ya kinadada ilikuwa ndogo sana. Katika ulimwengu huu wa Bitcoin, wengi bado wanaamini ni fursa ya wanaume pekee na huu ni mtazamo usio sahihi.
Tunahitaji kuwa na uwiano. Tunahitaji kinadada waamke na wajifunze hii teknolojia. Tunaweza kujifunza kutoka kwa majirani zetu Kenya 🇰🇪, ambako kuna hamasa kubwa na jumuiya imara za wanawake kwenye industry kama BTC Dada, DadaDevs, Women in Blockchain na nyingine nyingi.
Kuna fursa nyingi sana ndani ya Bitcoin kwa kinadada kama waelimishaji, developers, designers, entrepreneurs na viongozi.
Hitimisho: Teknolojia hii ni kwa ajili yetu sote. Tukishirikiana wanaume na wanawake kwa pamoja, tukiwa na umoja na malengo ya pamoja, tutafika mbali zaidi na kujenga Tanzania ya kidijitali inayomilikiwa na Watanzania wenyewe. Ni wakati wa dada zetu kuamka!
#bitcoin.” #hrf #lightningnetwork #BitcoinEducation #BTC