FAHAMU KWA HARAKA - Blockchain Explorer

Umewahi kutuma crypto halafu ukaanza kuwaza:

“Hii pesa imefika kweli au imepotea njiani?”

Usijali… kuna “Google” ya blockchain inayokuonyesha kila kitu LIVE.

Fikiria umetuma pesa kwa M-Pesa.

Unapata SMS kuthibitisha, sio?

Sasa kwenye crypto hakuna SMS…

Lakini kuna kitu kinaitwa Blockchain Explorer.

👉 Hii ni kama Google ya crypto

👉 Inakuonyesha:

- Pesa imetoka wapi

- Imeenda kwa nani

- Imefika au bado ipo njiani

Kwa lugha rahisi kabisa:

Blockchain Explorer = sehemu ya kuangalia ukweli wa miamala ya crypto.

👉 Hatua ya 1: Chagua explorer sahihi

- Bitcoin → Mempool.space

- Ethereum → Etherscan

- BNB Chain → BscScan

👉 Hatua ya 2: Fungua website yao

👉 Hatua ya 3: Copy ile TXID (Transaction ID) kutoka wallet yako

👉 Hatua ya 4: Paste kwenye search bar

👉 Hatua ya 5: Angalia majibu

Utaona:

- Status → Confirmed au Pending

- Amount → Kiasi kilichotumwa

- From & To → Imetoka na imeenda wapi

- Fee → Umechajiwa kiasi gani

Umetuma USDT kwa mtu wa Dar.

Anasema hajapokea.

Badala ya kubishana:

👉 Fungua explorer

👉 Angalia transaction

Ukweli utaonekana hapo hapo:

Kama imefika → yeye anakudanganya 😅

Kama haijafika → network bado ina-process

#CryptoRally #blockchain #explore #USDT